FAHAMU UBORA WA SIMU MPYA YA TECNO ( TECNO CAMON 30 )

Tangu mwezi wa nne kampuni ya walitoa matoleo ya Tecno Camon 30 Matoleo ya Camon 30 yapo matatu ambayo ni ya daraja la kati yaani mid range Ubora wa kiujumla uliopo kwenye simu zote tatu ni kasi kubwa ya kuchaji, mfumo endeshi wa HIOS 14 uliowezesha AI(akili mnemba) Tutaangalia baadhi ya vitu vilivyomo kwenye hios 14 Na kingine ni kwamba simu zote zinakuja na memori kubwa za kuanzia GB 256 Tuzame kiundani. Bei za Tecno Camon 30 SIMU Tecno Camon 30 690,000/= Tecno Camon 30 Pro 990,000/= Tecno Camon 30 Premier 1,250,000/= Ubora wa software Simu zote yaani Tecno Camon 30, Tecno Camon 30 Pro na Tecno Camon 30 Premier zinatumia mfumo endeshi wa Android 14 Na pia inaambatana na mfumo wa Tecno wa HIOS 14 HIOS 14 inakuja na vitu vingi vya artificial intelligence yaani akili bandia Cha kwanza kuna kinaitwa AI Eraser
Fikiria upo mtaani unapiga picha, kwenye mtaa kuna watu wanapita kwa nyuma Ukaja kugundua wapita njia wametokea kwenye picha yako na wewe hutaki AI Eraser ina uwezo wa kuwaondoa hao watu bila kuharibu uhalisia wa muonekano wa picha Kitu kingine ni kutengeneza wallpaper unayotaka wewe
Camon 30 Premier zitakupa ufanisi stahiki zaidi Betri na chaji Simu zote zina betri zenye ukubwa wa 5000mAh na chaji ya wati 70 Kama una haraka ya kwenda sehemu na simu yako haina chaji Unahitaji dakika 45 kuijaza betri lote kutoka 0 hadi 100 Camon zote zinajitahidi kutunza chaji hata katika matumizi ya intaneti Kiwastani, na kwa majaribio mbalimbali ukiwa kwenye intaneti simu inakaa karibu masaa 11 kwa kuperuzi Ila kama ni mchezaji wa gemu utadumu na chaji kwa masaa saba Ubora wa kioo Simu zote zinatumia kioo cha Amoled ila kioo cha tecno camon 30 premier ni kizuri zaidi Tecno Camon 30 na camon 30 premier zinakuja na skrini ya refresh rate inayofika 120Hz Ila Camon 30 Pro inafika hadi 144Hz Premier ina ubora wa ziada kwa sababu kioo chake ni cha LTPO AMOLED kikiwa na HDR Kioo cha namna hii kinadhibiti kiwango cha refresh rate chenyewe na kinaonyesha vitu kwa mkolezo sahihi Ila Tecno walipaswa waweke angalau HDR10+ Kamera Tecno Camon 30 Premier inakupa mfumo mzuri wa kamera kuliko camon 30 zingine Kwa mfano Camon 30 ina kamera mbili moja ina 50MP na OIS huku ya pili ikiwa na 2MP ambayo depth sensor Depth sensor huwa ni kamera inayopima eneo na kina cha kitu kinachopigwa picha Hivyo haipigi picha na haina umuhimu kwa sababu teknolojia za PDAF zinafanya hiyo kazi Camon 30 Premier ina lenzi za ultrawide na wide Wakati premier ina kamera muhimu za tekephoto, ultrawide na wide Na Pro na Premier zinarekodi video za 4K #tecnoCamon30 #tecno

Comments

Popular Posts