META KUJA NA MFUMO WA FACE ID KWA AKAUNTI ZA INSTAGRAM NA FACEBOOK'S

Meta imethibitisha inajaribu mfumo unaofanana na Face ID. Instagram na Facebook zimeanza majaribio ya kuweka kipengele kipya na mfumo mpya wa kutumia teknolojia ya utambuzi wa sura kusaidia watumiaji kurejesha akaunti zao mara moja endapo zitafungwa. Mfumo huu utatumika pia kuthibitisha mmiliki wa akaunti ni nani. Mchakato unahusisha kuchukua video ya selfie, ambapo unatakiwa kuzungusha kichwa chako kwa pande mbalimbali, kama vile unavyojisajili kwa Face ID. Watumiaji watakuwa na chaguo la kutumia utambuzi wa sura moja kwa moja au kupitia ukaguzi wa kibinadamu. Taarifa kutoka kwenye video hiyo ya selfie zitalindwa na kuwa encrypted, zitahifadhiwa kwa usalama, na kufutwa mara tu mchakato unapokamilika. Pia, teknolojia hii inatumika kugundua na kuzuia akaunti ambazo zinatumia picha za watu maarufu bila ruhusa yao. Na Meta itatumia sura ya kwenye akaunti katika picha zilizopo mtandaoni na matangazo. ______________ #Meta #Facebook #Instagram

Comments

Popular Posts